Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Amchoma visu mke mpaka kumuua

Amchoma Visu Mke Mpaka Kumuua Amchoma visu mke mpaka kumuua

Tue, 9 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi la Jimbo la Adamawa limemkamata mwanaume mwenye umri wa miaka 33 aliyetambulika kama Ibrahim Abubakar, kwa kumuua mke wake wa miaka 25, HajaraSa'adu.

Mshukiwa ambae ni Mchinjaji na mkazi wa Sabon Gari-Futy katika eneo la serikali ya mtaa wa Girei, Nigeria alimuua marehemu kwa kumchoma kisu kikali mgongoni na hivyo kumsababishia majeraha mabaya yaliyosababisha kifo chake.

Afisa Uhusiano wa Kamanda wa Jimbo SP Suleiman Yahaya Nguroje katika taarifa yake kwa vyombo vya habari alibainisha kuwa mshukiwa alimuua marehemu mnamo Aprili 8 majira ya saa 4:30 asubuhi, baada ya kumshutumu kwa kumnyang'anya simu yake ili kuangalia mawasiliano yake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live