Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ambundo aikamua Gor Mahia mamilioni

Ambundo Pic 1 Data Ambundo aikamua Gor Mahia mamilioni

Fri, 18 Dec 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Thomas Ng'ituMore by this Author WINGA Dickson Ambundo anayeichezea Dodoma Jiji anadaiwa kuikamua zaidi ya Sh. 20 milioni klabu ya Gor Mahia inayoshiriki Ligi Kuu Kenya.

Pesa hizo zinatokana na madai ya malimbikizo yake ya mishahara wakati anaichezea kwa mkopo klabu hiyo akitokea Alliance kabla ya Julai mwaka huu kuachana na timu hiyo.

Fifa kupitia taarifa yake, imewataka Gor Mahia kulipa pesa hizo (Sh.1.3 milioni za Kenya) ndani ya siku 45, kama wakishindwa kufanya hivyo watakutana na kifungo cha kutosajili hadi watakapomlimpa.

Ambundo ambaye sasa anaichezea Dodoma Jiji, aliondoka Gor baada mabingwa hao wa Kenya kuyumba kichumi kutokana na kujitoa kwa wadhamini wa ligi kampuni ya kubashiri ya SportPesa.

Malimbikizo ya mshahara wa Ambundo kutokana na mshahara wake kule ni Dola 1,200 ambayo ni ya kuanzia Septemba 1,2019 hadi Juni 1,2020.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz