Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ambokile ana jambo lake Mazembe

Ambokile+pic Ambokile ana jambo lake Mazembe

Fri, 6 Nov 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By OLIPA ASSASTRAIKA wa TP Mazembe, Mtanzania Eliud Ambokile amesema  pamoja na kutopata nafasi ndani ya timu hiyo, amekiri kufaidika na misingi mizuri inayompa mwanga wa namna gani awe mchezaji mkubwa.

Ambokile ameliambia Mwanaspoti Online leo Ijumaa, Novemba 6, 2020 kwa njia ya simu akiwa nchini Congo, kwamba ni kweli tangu ajiunge na TP Mazembe 2019 imekuwa ngumu kupata nafasi ya kucheza,  lakini hilo halijamzuia kujifunza mengi ya kiufundi, anayoona yatamsaidia kadiri siku zinavyokwenda.

Amesema soka la Congo lipo juu, kwamba wachezaji wengi wana ndoto za kucheza Ulaya ambapo Shirikisho la Mpira wa miguu Congo, limeweka mikakati ya kuwawezesha kutimiza hilo.

"Wenzetu wapo juu mpaka miundo mbinu yao, hivyo kutokucheza sio kwamba akili yangu imelala, najifunza kwanini wapo kiwango cha juu, aina gani ya soka wanacheza, aina ya mazoezi yao, mbinu na ufundi," amesema Ambokile na ameongeza kuwa

"Kuna siku ninachofanya kwa sasa kitaonekana uwanjani baadae, soka linahitaji uvumilivu wa hali ya juu ili kuweza kuishi kile ninachokitamani kiwe kwenye maisha yangu,"amesema.

Ambokile amesema mbali na kujifunza amekuwa akitiwa moyo na wachezaji wanaopata nafasi kikosi cha kwanza, wanaomwambia hata wao walipambana mpaka kufikia mafanikio yao.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz