Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Amalizwa na COVID-19 Saa Chache Baada ya Kutabiri Kifo Chake Facebook

B6fe3039c0e7c263 Amalizwa na COVID-19 Saa Chache Baada ya Kutabiri Kifo Chake Facebook

Thu, 1 Apr 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Tony Weru siku ya Jumanne, Machi 30, alikimbizwa katika Hospitali Kuu ya Wilaya ya Nyeri baada ya kukumbana na matatizo ya kupumua

- Usiku huo, alichapisha ujumbe kwenye kundi la Facebook la Digital Farmers akisema ameambukuziwa COVID-19

- Dakika chache baadaye alichapisha ujumbe wa kuwaaga wanachama wa kundi hilo

Kijana mjasiriamali kutoka Mweiga, kaunti ya Nyeri, ameaga dunia saa chache baada ya kutabiri kifo chake kwenye Facebook.

Tony Weru siku ya Jumanne, Machi 30, alikimbizwa katika Hospitali Kuu ya Wilaya ya Nyeri baada ya kukumbana na matatizo ya kupumua na aliwekwa kwenye oksijeni.

Usiku huo, alichapisha ujumbe kwenye kundi la Facebook la Digital Farmers akisema ameambukuziwa COVID-19 na hafahamu namna alivyopata.

"COVID-19 ni kweli ipo, endapo nitafariki. Sijui ni wapi nilipata," aliandika.

Dakika chache baadaye alichapisha ujumbe wa kuwaaga wanachama wa kundi hilo.

"Ninawaacha kupitia COVID-19," alisema huku akichapisha picha yake akiwa amevaa maski na kuonekana kulowa jasho.



Kufikia saa sita ya usiku alithibitishwa kufariki.

Katika kundi hilo lenye wanachama 430,000, marehemu alifamika kwa ukulima wake wa matunda ya strawberry na nyuki.

Katika taarifa tofauti TUKO.co.ke ilikuwa imeripoti kisa cha aina hii ambapo Mkenya mwingine alitabiri kifo chake mwezi Oktoba 2020 na akafariki mwezi mmoja baadaye.

Kelvoh Kanambo alikuwa ameandika ujumbe tatanishi kwenye mtandao wa Facebook Oktoba 29 na akafariki dunia Novemba 17 baada ya kuugua kwa muda mfupi.

"Hey guys kuna place nataka kuenda hivi karibuni, Nitawamisi sana lakini msijali nitakuwa nakuja kuwasalimia tu," aliandika.

Kanambo alizikwa nyumbani kwao eneo la Tetu, kaunti ya Nyeri.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke