Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyevuruga mipango ya Mudavadi kuwa Rais 2013 aomba radhi

3d6e25c82e656680 Aliyevuruga mipango ya Mudavadi kuwa Rais 2013 aomba radhi

Sun, 9 Jan 2022 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Gavana wa zamani wa Kiambu, William Kabogo amefunguka kuhusu namna alimshawishi Rais Uhuru Kenyatta kumtema kiongozi wa chama cha Amani National Congress (ANC), Musalia Mudavadi.

Kabogo amefichua kuwa ndiye alibuni njama ya kuvuruga mpango wa Mudavadi kuwania urais mwaka 2013Alitoboa siri kuwa wakati wa mwaka huo wa uchaguzi, Uhuru alikuwa amekubali kuzika azma yake ya kuwania urais na kumuunga mkono Mudavadi.

Uhuru alikuwa amezika azma yake ya kuwania urais ili kushughulikia kesi iliyokuwa inamwandama katika mahakama ya ICCLakini Kabogo hakufurahishwa na Uhuru kumpendelea Mudavadi kuwania urais na hivyo alimshinikiza rais amteme

Akizungumza siku ya Jumapili, Januari 9, wakati wa ibada katika Kanisa la RGC Liberty Christian Centre, kiongozi huyo wa chama cha Tujibebe Wakenya alifichua kuwa ndiye alibuni njama ya kuvuruga mpango wa Mudavadi kuwania urais mwaka 2013.

Uhuru alikuwa anamuunga mkono Mudavadi kuwania uraisKabogo alitoboa siri kuwa wakati wa mwaka huo wa uchaguzi, Uhuru alikuwa amekubali kuzika azma yake ya kuwania urais na kumuunga mkono Mudavadi.

Lakini Kabogo hakufurahishwa na Uhuru kumpendelea Mudavadi kuwania urais na

hivyo alimshinikiza rais awe mrithi wa Mwai Kibaki na kumtema mwenzake wa ANC.

Uhuru alikuwa amezika azma yake ya kuwania urais ili kushughulikia kesi iliyokuwa inamwandama katika mahakama ya ICC lakini alisukumwa na viongozi wa Mlima Kenya wakiongozwa na Kabogo.

Lakini sasa Kabogo anajutia vitendo vyake na kumuomba msamaha Mudavadi akisema anaweza kuhudumu katika cheo chochote ikiwemo kuwa naibu wake.

"Naomba unisamehe. Huo haukuwa wakati wako, wako utafika.Ninaweza kuhudumu kwa wadhifa wowote. Ninaweza kuhudumu kama naibu (rais) wa mtu mwema kama huyu," alisema huku akimnyooshea kidole Musalia.

Akihutubu katika ibada hiyo, Mudavadi alisema tukio hilo la 2013 lilikuwa pio kubwa kwake kuwahi kushuhudia katika taaluma yake.

Kabogo pia aliandamana pamoja na Seneta wa Nairobi, Johnson Sakaja na kuombea Kenya amani.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke