Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyeshangilia Odinga kushindwa Urais achukuliwa hatua

WhatsApp Image 2022 09 08 At 2.jpeg Raila Odinga

Thu, 8 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Cliff Onrichi ameonekana kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii akishangilia kwa furaha Raila Odinga kushindwa urais nchini Kenya.

Kutokana na video hiyo kusambaa, imeonekana kuwa mwajiri wake wa Kampuni ya Mabasi Transline Classic hakupendezwa na tukio hilo.

Hivyo, kampuni hiyo imetoa barua ya kuwaomba radhi watu, kwa kitendo kilichofanywa na Cliff na kubainisha kuwa tayari amechukuliwa hatua za kinidhamu.

“Kwa wateja wetu wapendwa, tumefikiwa na video klipu inayozunguka kwenye mitandao ya kijamii, iliyofanywa na Cliff Onrich ambaye ni mfanyakazi wa kawaida anayeishi katika ofisi zetu za kituo cha afya.

Kama kampuni tunataka kujitenga na klipu hiyo na kueleza kuwa klipu hiyo ilifanywa kwa utashi wake binafsi na haiwakilishi mitazamo ya kampuni hivyo, hatua za kinidhamu zimechukuliwa dhidi yake.

Tunaomba radhi kwa kila mtu hususani kwa wateja wetu wathamini kutokana na kukasirishwa na klipu hiyo, kama kampuni tupo kwenye biashara na sio kwenye siasa, tutaendelea kutoa huduma bora zaidi kwa wateja wetu wote” mwisho wa kunukuu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live