Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyesakwa kwa mauaji ya Kimbari ya Rwanda alifariki miaka 25 iliyopita - UN

Aliyesakwa Kwa Mauaji Ya Kimbari Ya Rwanda Alifariki Miaka 25 Iliyopita   UN Aliyesakwa kwa mauaji ya Kimbari ya Rwanda alifariki miaka 25 iliyopita - UN

Wed, 15 Nov 2023 Chanzo: Bbc

Umoja wa Mataifa umethibitisha kifo cha Aloys Ndimbati, mtuhumiwa mauji ya ki aliyesakwa sanakwa uhalifu wa mauaji ya kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994 alifariki miaka 25 iliyopita.

Katika taarifa yake, kitengokinachoshughulikia kesi zilizoachwa na Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda mjini Arusha (ICTR), kinasema kuwa Aloys Ndimbati alifariki dunia mwishoni mwa Juni mwaka 1997.

Kitengo hichokinasema kwamba ilichukua miaka hiyo yote ya mashauri kabla ya kufikia uamuzi kuwa alifariki.

Ndimbati alishtakiwa kwa makosa saba ya mauaji ya halaiki, uhalifu ambao inasemekana aliufanya katika manispaa ya Gisovu, ambako alikuwa mbabe wakati wa mauaji ya kimbari.

Kulingana na kitengo hicho , Ndimbati alifariki mwishoni mwa Juni mwaka 1997,katikakijiji chaGatore katika wilaya ya Kirehe jimbo la Mashariki mwa Rwanda.

Taarifa Zaidi zinasema kwamba alikuwa amerejea mwezi Junimwaka 1997 kutoka Zaire (sasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo), ambako alikuwa amekimbia na familia yakemwezi Julai ,1994, baada ya mauaji ya kimbari.

Hata hivyo, tangu alipowasili katika kijiji cha Gatore, hakuna taarifa zozote kumhusu zilizojulikana, isipokuwa uchunguzi wa Umoja wa Mataifa unathibitisha kwamba hakuondokamahali hapo.

Kutokana na hali yamtafaruku uliokuwepo wakati huo, taarifa hiyo inasema kuwa haikufahamika ni kwa namna gani Aloys Ndimbati alifariki.

Shirika la Umoja wa Mataifa, hata hivyo, linasema kuwa kifo hicho kimethibitishwa na ofisi ya mashtaka ya Rwanda katika uchunguzi wake.

Wakati wa mauaji ya kimbari, Aloys Ndimbati alikuwa mkuu wa wilaya ya Gisovu katika mkoa wa zamani wa Kibuye. Hapo ndipo inasemekana aliamuru mauaji ya Watutsi.

Chanzo: Bbc