Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyepoteza wazazi akiwa na miaka 5, akakatwa mkono ahitkmu uanasheria

Operanews1670593224676 Aliyepoteza wazazi akiwa na miaka 5, akakatwa mkono ahitkmu uanasheria

Fri, 9 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Simulizi ya mwanaume mmoja ambaye alipoteza mkono akiwa na umri wa miaka 10 imesisimua wengi mitandaoni.

Mwanaume huyo ambaye alikiuka maneno ya shaka kutoka kwa watu na kufuzu kama wakili alipoteza wazazi wake akiwa na umri wa miaka 5 tu.

Dominic Akpan alisimulia hadithi ya maisha yake kupitia ukurasa wake wa Facebook na kuwaaminisha wengi kuwa hakika hakuna lisilowezekana chini ya jua pakiwemo na nia na moyo wa kujituma.

Akpan alisimulia hadithi hiyo aliyoipa mada kuwa ‘Nilifanya udhubutu’ na kusema kuwa alipoteza mamake akiwa na miaka 4, babake akafuata mwaka mmoja baadae akiwa na miaka 5 na alipofika miaka 10 akapoteza mkono.

“NILITHUBUTU KUWA, LEO NIMEKUWA MIMI. Yangu ni hadithi ya neema na uamuzi kamili wa kibinafsi. Kutoka kwa kupoteza; Mama yangu nikiwa na miaka 4, Baba yangu nikiwa na miaka 5, Kiungo changu cha juu cha kulia nikiwa na miaka 10. Hadi Kwa; Kuwa Mwanasheria na Wakili wa kwanza wa Mahakama Kuu ya katika familia yangu,” Akpan alisimulia.

Hakuna hasara yoyote kati ya hizi isiyoweza kurekebishwa iliyomzuia Akpan kufuata ndoto zake kwani bado alienda mbele kusomea sheria na kuhitimu. Alisema hadithi yake inaashiria dhamira na kwamba alithubutu kujaribu licha ya shida zote.

Alisema kuwa hadithi yake hawezi kujivuna bali ni kwa uwezo wa Mungu tu na neema ya kutaradadi katika maisha yake yote.

“Imekuwa MUNGU, FAMILIA yangu na MARAFIKI, na siku moja hivi karibuni, natumai kusimulia hadithi yangu. Lakini kabla ya hapo, niruhusu nijitambulishe tena, Mimi ni I. D. AKPAN ESQ,” aliandika.

Hadithi ya Akpan ilisambaa mara moja kwani ilichapishwa tena na watumiaji wengine wa Facebook ambao walitaka kusherehekea naye.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live