Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyepotea Kenya akutwa na kifo Uganda

Police Line Do Not Cross Police Sirens In The Background Caution Tape With A Police Car Video Police Line

Wed, 4 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanaume mmoja Raia wa Kenya Paul Mutai Koshior, 57 amepatikana ameuawa na mwili wake kutupwa katika shamba la mahindi katika Wilaya ya Bukwo,nchini Uganda.

Kifo chake kimethibitishwa na mwanawe wa kiume, Kibiwott Kamoo, ambaye alimpigia simu siku chache kabla ya kutoweka kwake,baada ya kadi ya mpiga kura na picha za passport zenye majina yake kukutwa pembeni ya mwili wake.

"Nilipigiwa simu na mtu mmoja ambaye alijitambulisha kama afisa wa Polisi kutoka Kituo cha Polisi cha Suam nchini Uganda na alinipa taarifa ya kifo cha baba yangu,alisema mwili wake ulikuwa umetupwa katika shamba la mahindi na ulipatikana na mkazi wa wilaya ya Bukwo,” Kamoo alisema.

Vyombo vya Usalama nchini Uganda vimesema vinaendelea na uchunguzi kuweza kufahamu ni kina nani waliohusika katika tukio hilo na mara tu watakapofahamu familia yake itapewa taarifa na wahusika watafikishwa mbele ya vyombo vya Sheria.

Paul alitoweka nyumbani kwake maeneo ya Eldoret,Kaunti ya Uasin Gishu nchini Kenya Julai 19 mwaka huu, na mwili wake kupatikana umetelekezwa katika Wilaya ya Bukwo,nchini Uganda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live