Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyepanda Kilimanjaro kusisimua akili afika fainali ya tennis

93802 Tenis+pic Aliyepanda Kilimanjaro kusisimua akili afika fainali ya tennis

Fri, 31 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Melbourne, Australia. Mcheza tennis nyota duniani, Garbine Muguruza, ambaye aliamua kupanda Mlima Kilimanjaro ili kusisimua akili baada ya kuwa na matokeo mabaya mfululizo, amefanikiwa kutinga fainali ya michuano ya wazi ya Australia. Muguruza alipambana kushinda seti zote baada ya kutanguliwa mara mbili na Simona Halep jana Alhamisi na sasa atakutana na Sofia Kenin katika fainali. Mchezaji huyo wa Hispania, ambaye ameshashinda vikombe viwili vya mashindano makubwa ya tennis (Grand Slam), amefika fainali yake ya kwanza ya Melbourne kwa kushinda kwa michezo 7-6 (10/8) na 7-5 katika mechi iliyofanyika uwanja wa Rod Laver Arena. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 ambaye kiwango chake kiliporomoka sana msimu uliopita, ni mchezaji wa kwanza ambaye hakuwa katika orodha ya ubora kwa michuano hiyo, kufika fainali tangu mafanikio hayo yafikiwe na mchezaji wa Ubelgiji, Justine Henin mwaka 2010. "Ni furaha sana kufika fainali, ni safari ndefu na nina mechi moja zaidi Jumamosi," alisema Muguruza, ambaye alikuwa mchezaji nambari moja kwa ubora duniani lakini sasa anashikilia nafasi ya 32. Muguruza alitwaa ubingwa wa mashindano ya wazi ya Ufaransa mwaka 2016 na Wimbledon mwaka uliofuata, lakini kiwango kikaporomoka na kujikuta akifikia hadi nafasi ya 32 kwa ubora duniani. Msimu uliopita, Muguruza alitolewa katika mashindano mawili ya Grand Slam ya Wimbledon na US Open, na baadaye akaamua kujaribu kitu kiingine tofauti ili kujiandaa namsimu wa mwaka 2020. "Unapanda huo mlima (Kilimanjaro) na unakuwa peke yako. Hupati kombe lolote, zawadi yoyote, wala picha, hakuna kitu kule juu," alisema Muguruza akizungumzia siku chache za Novemba alizotumia kupanda mlima huyo mrefu kuliko wote barani Afrika. "Ni changamoto halisi kimwili na kiakili kufika kule na nilikuwa naangalia kitu cha kufurahisha, kupata uzoefu tofauti nje ya mchezo wa tennis." Kwa mtu ambaye hapendi hali ya hewa ya ubaridi, anakiri Muguruza, angeweza kuwa na wazo tofauti wakati akipanda mlima kilimanjaro. "Sikupata shida kule na timu yangu na kupanda na kuwa chini ya hali ya hewa chini ya nyuzi sifuri na wakati wa usiku," alisema. "Wakati fulani inakuwa kama unajiuliza, 'nafanya nini huku?'" Na alirejesha kiwango chake baada ya kurejea. Katika mashindano ya kufungulia msimu ya Shenzhen nchini China alishinda mechi zake kwa mara ya kwanza tangu wakati wa mashindano ya French Open yaliyofanyika Mei-Juni, kabla ya kutolewa katika nusu fainali na sasa amefika fainali ya mashindano ya Australia.

Chanzo: mwananchi.co.tz