Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyenaswa chini ya jengo lililoporomoka Afrika Kusini atuma ujumbe kwa familia

Aliyenaswa Chini Ya Jengo Lililoporomoka Afrika Kusini Atuma Ujumbe Kwa Familia Aliyenaswa chini ya jengo lililoporomoka Afrika Kusini atuma ujumbe kwa familia

Wed, 8 May 2024 Chanzo: Bbc

Miongoni mwa wale ambao bado wamenasa chini ya vifusi baada ya jengo la ghorofa tano kuporomoka nchini Afrika Kusini ni Delvin Safels, ambaye alikuwa kwenye moja ya orofa za chini wakati jengo hilo linapoporomoka, babake Dion aliambia BBC.

Waokoaji wamefuatilia eneo la Delvin lakini wanatatizika kumfikia.

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 29 amekuwa akiwatumia ujumbe wa sauti wazazi wake na mpenzi wake, Aliyenaswa chini ya jengo lililoporomoka Afrika Kusini atuma ujumbe kwa familiaakiwaambia jinsi anavyowapenda.

Ana maumivu, na mkono na mguu umefungwa chini, na ni baridi na giza.

"Ninaamini mwanangu atatoka akiwa hai," baba yake Dion alisema.

Amekuwa akipiga kambi eneo la tukio karibu tangu Jumatatu, akitumai kwamba mtoto wake angepatikana. Anayumba kati ya kukata tamaa na tumaini.

"Ni kijana mwenye nguvu, nadhani ataokolewa usiku wa leo au hivi karibuni."

Zaidi ya siku moja baada ya jengo la ghorofa kuporomoka, waokoaji bado wanasaka watu 41 ambao bado hawajulikani walipo katika mji wa pwani wa kusini wa George.

Aliyenaswa chini ya jengo lililoporomoka Afrika Kusini atuma ujumbe kwa familia

Takriban watu 34 hadi sasa wameondolewa kwenye vifusi, saba kati yao wamethibitishwa kufariki.

Manusura na wapendwa wa watu wengine ambao bado wamenaswa bado wamesalia kwenye eneo la tukio.

Chanzo: Bbc