Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyemuua mkewe kisa kupokea simu usiku akamatwa

SIMU Mwanaume Aliyemuua mkewe kisa kupokea simu akamatwa

Thu, 23 Jun 2022 Chanzo: TUKO

Mwanamume mmoja kutoka kaunti ya Kilifi anayehusishwa na mauaji ya mkewe ametiwa mbaroni na sasa anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Mtwapa.

Mwanaume huyo ambaye ni dereva wa lori anadaiwa kurejea kutoka safarini na kufanya kitendo hicho cha kinyama baada ya mkewe kupokea simu majira ya saa sita usiku.

Ripoti ya NTV ilionyesha kuwa, Lulu Ibrahim mwenye umri wa miaka 29 ambaye alikuwa mama wa watoto sita, alikata roho kutokana na majeraha mabaya aliyopata.

Ndugu zake walishindwa kustahimili uchungu wao walipoupokea mwili wa jamaa yao na kulaani tukio hilo wakijutia kutokuwa na imani kubwa kati ya mume na mkewe.

Chanzo: TUKO