Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyekuwa Waziri wa Michezo Hassan Wario afungwa jela miaka 6

5a98ca6a81bc91e3 Aliyekuwa Waziri wa Michezo Hassan Wario afungwa jela miaka 6

Thu, 16 Sep 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Aliyekuwa Waziri wa Michezo Hassan Wario na aliyekuwa afisa wa Kamati ya Olimpiki ya Kitaifa ya Kenya (Nock) Stephen Soi, wamepatikana na hatia ya ufisadi na matumizi mabaya ya mamlaka kuhusiana na kashfa ya Olimpiki ya Rio 2016.

Mwanadiplomasia huyo ana siku 14 kukata rufaa kuhusiana na uamuzi wa mahakama baada ya kupatikana na hatia ya utovu wa nidhamu akiwa waziriAnakabiliwa na mashtaka ya matumizi mabaya ya mamlaka chini ya Sheria ya Kupambana na Rushwa na Uhalifu wa Kiuchumi.

Wario na aliyekuwa afisa katika Kamati ya Michezo Kenya (NOCK) Stephen Soi walizuiliwa Gigiri mnamo Jumatano, huku wakisubiri uamuzi ma kortiWaziri huyo wa zamani sasa ametozwa faini ya KSh 3.6 milioni au kutumikia kifungo cha miaka sita gerezani.

Wario amehukumiwa kifungo cha miaka sita jela au kulipa faini ya KSh 3.6 milioni kwa kuhusika kwake katika kashfa hiyo.

Soi kwa uoande wake anakodolea macho kifungo cha miaka 10 jela au faini ya KSh 103 milioni kwa madai ya matumizi mabaya ya pesa za umma.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke