Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyekuwa Spika wa Nairobi Alex ole Magelo afariki dunia

Ae0b84de6423704c Aliyekuwa Spika wa Nairobi Alex ole Magelo afariki dunia

Wed, 5 May 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Magelo aliwahi kuhudumu kama mwenyekiti wa AFC Leopards na pia Spika wa kaunti ya Nairobi

- ALiangamizwa Jumanne Mei 4 na makali ya coronavirus baada ya kuugua kwa muda

- Rais Kenyatta wakati wa hotuba ya Mei alisema ugonjwa huo ungali tishio kubwa kwa Wakenya

Aliyekuwa Spika wa kaunti ya Nairobi Alex ole Magelo ameaga dunia baada ya kuugua kwa muda.

TUKO.co.ke imefahamishwa kuwa Magelo aliangamizwa na makali ya virusi vya corona baada ya kukabiliana navyo kwa muda.

Magelo alihudumu katika serikali ya kaunti ya Nairobi kuanzia 2013 wakati chama cha ODM kilikuwa kikiwika humo.

Alichukua nafasi hiyo baada ya kuchaguliwa na MCAs 43 dhidi ya 42 wa Jubilee ambao walikuwa wakimuunga mkono Mutanga Mutungi.

Atakumbukwa pia kwa kuhudumu kama mwenyekiti wa klabu cha mpira cha AFC Leopards humu nchini.

Mtangazaki wa soka Carol Radull ni baadhi ya wale ambao waliomboleza kifo cha kiongozi huyo mtandao.

"Aliyekuwa mwenyekiti wa AFC Leopards na Spiak wa kaunti ya Nairobi Alex ole Magelo amefariki kutokana na Covid-19. Pumzika salama rafiki yangu," Radull alisema.

Magelo anaingia kwenye idadi ya watu mashuhuri waliomalizwa na maradhi hayo ambayo yanatishia mataifa mengi.

Rais Uhuru Kenyatta amekuwa akiwataka Wakenya kuzingatia sheria zilizotolewa na Wizara ya Afya kukabili janga hilo.

Wakati wa hotuba yake ya Mei 1, Rais alisema yuko radhi kufanya kila serikali iwezalo kuyalinda maisha ya wananchi.

"Wajibu wangu wa kwanza ni kulinda maisha. Na niko radhi kufanya kila liwezekanalo ili kuhakikisha tunayaokoa maisha. Hatutaki kupatwa na yale tunashuhudia katika mataifa mengine," alisema Rais.

Tayari viongozi kadhaa wakiwamo waliochaguliwa wameangushwa na makali ya coronavirus.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama habari za TUKO hapa

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke