Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyekuwa Rais wa Ivory Coast amuomba mkewe wa miaka 32 talaka

104bd2a0599394e2 Aliyekuwa Rais wa Ivory Coast amuomba mkewe wa miaka 32 talaka

Thu, 24 Jun 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Punde baada ya kuondolewa kesi na Mahakama ya Kimataifa kuhusu Uhalifu (ICC), Laurent Gbagbo aliwasilisha kesi ya talakaRais huyo wa zamani wa Ivory Coast anataka kuvunja ndoa yake ya miaka 32 na Simone Uhusiano wa Gbagbo na Simone umekuwa na doa na sasa kiongozi huyo anachumbiana na mwanahabari wa zamani

Rais wa zamani wa Ivory Coast, Laurent Ggabo amewasilisha ombi la kupewa talaka na mke wake.

Katika taarifa iliyotolewa Juni 21, 2021, wakili wa Gbagbo alisema rais huyo wa zamani ameamua kitengana na mke wake Simone baada ya miongo mitatu pamoja.

Tangazo hilo linakjia siku chache baada ya Gbagbo kurejea Ivory Coast akitokea Mahakama ya Kimataifa kuhusu Uhalifu (ICC), nchini Netherlands.

Aliondolewa kesi ya uhalifu kufuatia ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2010.

Penyenye zimekuwa zikidai kwamba uhusiano wa Gbagbo na Simone umekuwa na doa na.

Wawili hao walikula viapo vya ndoa mwaka 1989 na kisha kubuni pamoja chama cha Ivorian Popular Front, ambacho kilishinda chaguzi za mwaka 2000 baada ya miaka kadhaa upinzani.

Wakati Gbagbo alikataa kushindwa baada ya chaguzi za 2010, wengi waliamini kuwa Simone ndiye alichochea uamuzi huo.

Baada ya wiki kadhaa ya vita, wafuasi wa Ouattara walivamia makazi ya Gbagbo na kumzuia pamoja na Simone.

Gbagbo anachumbiana na mwanahabari wa zamaniGbagbo anaonekana kusonga mbele na maisha yake huku akimtema Simone na anaripotiwa kuchumbiana na mwanahabari wa zamani Nady Bamba.

Kiongozi huyo wa zamani aliwasili Ivory Coast akiwa ameandamana pamoja na Bamba, na Simone ndiye alimpokea katika uwanja wa ndege.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 073248269.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke