Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyekua waziri wa mambo ya ndani Kenya Fred afika mahakamani

Aliyekua Waziri Wa Mambo Ya Ndani Kenya Fred Afika Mahakamani .png Aliyekua waziri wa mambo ya ndani Kenya Fred afika mahakamani

Thu, 9 Feb 2023 Chanzo: Bbc

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Kenya Fred Matiang'i ameenda mahakamani kwa madai ya kuvamiwa na polisi usiku wa manane nyumbani kwake eneo la Karen.

Mapema leo Alhamisi, mawakili wa Matiangi waliripoti kwamba polisi walijaribu kumkamata mteja wao kinyume cha sheria.

Mawakili hao walidai kuwa baadhi ya maafisa wa polisi watiifu kwa Waziri huyo wa zamani walimdokezea kuhusu kukamatwa kwake na hivyo kusababisha atoe tahadhari.

"...nimepokea taarifa za kuaminika kutoka kwa maafisa wa polisi wa Kenya kwamba wako chini ya maagizo ya moja kwa moja kumkamata kiholela kwa nia ya kufikishwa mahakamani kwa sababu za kisiasa".

Kwa hivyo, Matiang'i aliiomba mahakama kutoa maagizo ya kuwazuia polisi kumkamata au kumfungulia mashtaka.

Chanzo: Bbc