Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyejifungua watoto 9 kwa pamoja aonesha sura zao

01f54087ec386f12 Aliyejifungua watoto 9 kwa pamoja aonesha sura zao

Sun, 24 Oct 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Mnamo Mei 2021, Halima Cisse alijifungua watoto tisa kwa mkupuo mmoja na kumfanya kuwa mama wa watoto 10. Miezi sita baadaye, watoto hao wameondolewa kwenye mashine ya kuweka watoto waliozaliwa kabla ya kutimiza muda na wanaendelea kuwa na nguvu.

Mama huyo anayejivunia kuwa na watoto 10, alifichua nyuso zao na ni furaha kuwaona wakikuaMwanamke raia wa Mali ambaye alijifungua watoto tisa kwa mkupuo mmoja amefichua nyuso zao katika picha za kuvutia.

Halima Cisse mwenye umri wa miaka 26, alifungua watoto hao mnamo Mei mwaka huu na kuvunja rekodi iliyokuwa inashikiliwa na Nadya Suleman ambaye alizaa watoto wanane mwaka 2009.

Akizungumza na Daily Mail, mama huyo ambaye sasa ana watoto 10, alisema watoto wake wanaendelea kukua wakubwa na kupata nguvu na wako tayari kurejea nyumbani kwao nchini Mali.

Cisse alijifungua katika kliniki ya Ain Borja mijini Casablanca, Morocco, na watoto hao tisa wakiwemo wasichana watano na wavulana wanne waliwekwa kwenye mashine hadi Agosti.



"Wote wanaendelea vizuri sana, na ni furaha kuwatunza. Wanazidi kuwa na nguvu kila siku na inawezekana kuwa wataruhusiwa kuacha huduma ya matibabu wakati wowote ili tuweze kuwapeleka nyumbani," alisema

Halima na mume wake Kader Arby, 35, walisema japo ni furaha kuwatunza wanao, wanawazia jinsi watajipanga kimaisha ili waweze kuwalea wanao 10, pacha hao tisa watakaporejea nyumbani.



"Kuna mengi kwetu kuhangaika lakini tumejaa mawazo mazuri," aliongeza.

Kutokana na picha hizo zilizopakiwa, watoto wavulana walipewa majina Oumar, Elhadji, Bah na Mohammed VI.



Ilhali watoto wasichana watano walioviswa nguo zenye rangi ya waridi walipewa majina Adama, Oumou, Hawa, Kadidia, na Fatouma.

Serikali ya Mali pia imewasaidia sana wanandoa hao huku ikilipa bili ya hospitali.

Kama TUKO.co.ke ilivyoripotiwa awali, baada ya malaika hao kuzaliwa, daktari ambaye alimshughulikia Halima na wanawe alisema wana kibarua kigumu mbele yao.

"Bado kuna kazi ya kufanya kwa sababu ni mapema sana. Wanahitaji kupata uzito. Wanahitaji kunyonyeshwa. Kuna shida nyingi zinazotungojea," alisema.

Pacha hao walizaliwa na uzani wa kati ya kilogramu 0.5 na kilogramu moja baada ya uja uzito wa wiki 30 na iliwachukuwa madaktari 30 kuwazasilisha watoto hao salama.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke