Mfanyabiashara aliyewaiba watoto aliowadanganya ataenda kuwanunulia viatu amesukumwa jela miaka minne bila faini.
Scolastica Itula Kilonzo mwenye umri wa miaka 64 alihukumiwa jela na hakimu mwandamizi Charles Mwaniki baada ya kukutwa na hatia ya wizi wa watoto.
Itula alipatikana amewaficha watoto hao katika eneo la Kalawa, kaunti ya Machakos nchini Kenya. Mmoja wa watoto hao alifariki akiwa amefichwa na Itula.
Alipatikana na hatia ya kuwaficha watoto hao kwa mama yake mzazi kaunti ya Machakos. Inadaiwa kwamba Itula aliwaficha watoto hao kati ya Aprili 2011 na Desemba 2013.
Itula alishtakiwa aliwaiba watoto hao kutoka kwa Bennedetta Kasalu aliyekuwa amemwajiri kama yaya. Itula na mlalamishi walikuwa wakiishi pamoja katika mtaa wa mabanda wa Kibra, Nairobi.
Baada ya kuwapeleka huko Kalawa, mshtakiwa aliwapeleka shule na kuwaandikisha kama wanawe. Alipowaficha kwa mama yake mzazi, aliagiza Bi Kasalu asiruhusiwe kuwaona. Pia, aliagiza watoto hao wasikubaliwe kutoka nyumbani Kalawa.
Mshtakiwa alidai aliwaokota watoto hao baada ya kuachwa na mama yao lakini hakimu akamweleza hakupiga ripoti kwa polisi ama afisa anayehusika na masuala ya watoto.
Wandani wa Uhuru wasema hawajutii kuunga Azimio.