Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyeiba gari la Rais kwenye msafara ahukumiwa kifo

Bmw 735.jpeg BMW 736

Mon, 18 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanaume mmoja raia wa nchini Kenya ambaye anadaiwa kuiba gari la Rais Uhuru kenyata mwaka 2014 amehukumiwa kifo.

Mwanaume huyo anadaiwa kuiba gari aina ya BMW 735 ambalo lilikuwa na thamani ya dola za Kimarekani 10,200 kwa wakati huo na lilikuwa katika msafara wa rais na hiyo ni kwa mujibu wa vituo vya habari vya taifa la Kenya ambavyo viliripoti taarifa hiyo kwa mwaka huo.

Wakati akitoa hukumu hiyo hakimu mfawidhi wa mahakama ya Mlimani Francis amesema mtu huyo ambaye ni mtaalamu au fundi wa umeme amepewa adhabu hiyo kali kwa sababu ya vitendo vyake kuhusiana na usalama wa taifa.

Mwanaume huyo akiwa na wanaume wengine wawili walimpora Inspekta Mkuu wa Polisi David Machui kwa mtutu wa bunduki mnamo Agosti 26, 2014 katika Jiji la Nairobi nchini Kenya.

Inaelezwa kuwa watu hao walikuwa na bunduki aina ya Ak 47 na bastola nyingine wakati wa kutekeleza uhalifu huo, na huo ni kwa mujibu wa ushahidi uliowasilishwa mahakamani.

Watu hao wakaripotiwa kumvua nguo inspector huyo wa polisi na kumtelekeza katika kichaka.

Inaelezwa kuwa bwana huyo mara baada ya kuwa wamefanikisha jambo hilo alikwenda katika gereji moja iliyopo katika jiji la Nairobi na kisha kuondoa mfumo uliokuwa ukifanya gari hilo kufatiliwa na kuondoka zake kwenda Uganda.

Inaelezwa kuwa polisi wa Kenya kwa kushirikiana na polisi wa Uganda walianza msako kwa kumtumia mpenzi wake ambaye alikubali na kuanza kutengeneza miadi ya kukutana iliyofanikisha kukamatwa kwake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live