Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyechoma Bunge Afikishwa Mahakamani

Zandile Mafe Aliyechoma Bunge Afikishwa Mahakamani

Thu, 13 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MWANAUME kutoka Afrika Kusini aitwaye Zandile Mafe (49) amefikishwa Mahakamani akituhumiwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo la ugaidi baada ya kukamatwa maeneo ya Bunge la nchi hiyo muda mfupi baada ya Bunge kuwaka moto mnamo Januari 2, 2022.

Mafe amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Cape Town na anatuhumiwa kuchoma Bunge ambapo camera za CCTV zilimnasa akiwa maeneo ya Bunge. Anatuhumiwa pia kwa nia ya kutaka kuiba laptop na kumbukumbu nyingine muhimu za Kibunge.

Mwendesha mashitaka wa mahakama hiyo, Helene Booysen amepokea ripoti ya matibabu ikionyesha Mafe anasumbuliwa na tatizo la paranoid schizophrenia (ugonjwa wa akili) jambo ambalo linaweza kuifanya  kesi hiyo kukosa nguvu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live