Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Alichokisema Makamu wa Rais Tanzania Samia mkutano AU

95137 AU+PIC Alichokisema Makamu wa Rais Tanzania Samia mkutano AU

Mon, 10 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Addis Ababa. Tanzania imetaka Umoja wa Afrika (AU) na Jumuiya za Kimataifa kuongeza jitihada na nguvu ili kuleta amani katika maeneo yenye migogoro barani Afrika hususani nchi za Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Hatua hiyo itaipunguzia Tanzania mzigo wa wakimbizi ulioubeba kwa muda mrefu hivi sasa.

Hayo yamesemwa leo Jumapili Februari 9, 2020 na Makamu wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassani katika siku ya kwanza ya mkutano wa 33 wa kawaida wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika unaofanyika Addis Ababa nchini Ethiopia.

Amesema kauli mbiu ya mkutano wa mwaka 2020 kunyamazisha silaha umekuja wakati muafaka kwa kuwa mapigano na kutokuwapo utulivu katika baadhi ya nchi za Afrika zinachelewesha maendeleo katika bara hilo.

Samia amesema endapo Umoja wa Afrika na Jumuiya za Kimataifa zitaongeza nguvu katika kunyamazisha silaha na kukawapo amani na utengamano ni dhahiri viongozi wataelekeza nguvu kubwa  katika maendeleo endelevu ya wananchi hivyo kupunguza umasikini katika bara la Afrika ambalo linaonekana kama bara lililogubikwa na migogoro na mapigano.

Samia ameuahidi Umoja wa Afrika kuwa Tanzania itatekeleza kwa kasi mpango wa Umoja huo katika mapambano dhidi ya malaria na kwamba Tanzania imedhamiria kuutokomeza kabisa ugonjwa wa Malaria ifikapo mwaka 2030.

Pia Soma

Advertisement
Katika Mkutano huo wa 33 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika wameshuhudia mabadilishano ya uenyekiti ambapo Mwenyekiti anayemaliza muda wake, Abdel Fattah el-Sisi ambaye pia ni Rais wa Misri amekabidhi Uenyekiti kwa Rais wa Afrika ya Kusini, Cyrill Ramaphosa ambaye anakuwa mwenyekiti mpya wa Umoja wa Afrika.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz