Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Alichoagiza Rais Museveni kwa waasi wa ADF waliopo Uganda

WhatsApp Image 2021 08 15 At 3agg.jpeg Alichoagiza Rais Museveni kwa waasi wa ADF waliopo Uganda

Sun, 21 Nov 2021 Chanzo: BBC

Rais wa Uganda Yoweri Museveni anasema kundi la waasi, Allied Democratic Forces linastahili kujisalimisha huku akisisitiza kuwa serikali yake imejitolea kukabiliana na ugaidi.

Katika hotuba liliyorushwa moja kwa moja kwenye televisheni siku tano baada shambulio dhidi ya mji mkuu wa Kampala, Museveni alisema ADF wamejiamini sana kwa sababu wanaweza kutembea huru katika kambi za kijeshi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na wanajishughulisha na uchimbaji madini na biashara za mbao.

Hata hivyo amesema kuwa Uganda itaendelea kuwasaka wanachama wa kundi hilo na kuongeza kuwa ni vyema wale ambao hawajasalimisha silaha zao wafanye hivyo.

Wapiganaji ADF wanaofanya mashambulio Uganda ni akina nani? Islamic State, IS lilidai kuhusika na shambulio la Jumanne ambalo lilisababisha vifo vya watu wanne na kuwajeruhi wengine zaidi ya 30.

ADF katika miaka ya hivi karibuni na pia inajulikana kama Mkoa wa Afrika ya kati ya Islamic State.

Museveni amesema kuwa ADF sasa wamegeukia vitendo vya ugaidi katika maeneo ya mijini baada ya kushindwa katika eneo la Rwenzori na vijijini 2007.

Tangu mwezi Juni kufuatia jaribio la mauaji ya wiziri wa ngazi ya juu yanayoshukiwa kutekelezwa na waasi wa ADF, mashirikai ya usalama ya Ugand yamewaua washukiwa 12 na kuwakamata 's security agencies have killed 12 wengine 106. Miongoni mwa watano kati ya wale waliouawa ni mhubiri wa Kiislamu aliyefariki siku tano zilizopita.

Rais Museveni kwa sasa anafanya mazungumzo. Na mwenzake wa DRC, Rais Felix Tshiekedi juu ya uwezekano wa kupeleka wanajeshi wa Uganda mashariki mwa Kongo kupambana na kundi la waasi.

ADF ilianza vipi? Kikundi cha ADF kilianzishwa magharibi mwa Uganda ambapo kiliundwa na wanajeshi waliokuwa wakimuunga mkono rais wa zamani wa nchi hiyo Idi Amin, na kuanzisha vita vya kupambana na utawala wa rais wa sasa, Yoweri Museveni, kikundi hicho kikidai kuwa kuwa utawala huo umekuwa ukiwafanyia maasi.

Kikundi hiki kiliposhindwa na jeshi la Uganda mwaka 2001, kilihamia katika Kivu Kusini katika Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Baada ya kipindi kirefu cha kusitisha harakati zake, ADF ilisikika tena mwaka 2014 ilipoanza mashambulio ya mara kwa mara dhidi ya raia wa Congo.

Mwaka 2015, ndipo Musa Seka Baluku alipochukua uongozi wa kundi hili baada ya mtangulizi wake Jamil Mukulu kukamatwa .Bakulu alitangaza kujiunga na IS mwaka 2016.

Hatahivyo kikundi IS kilianza kutangaza kuwa inaendesha harakati zake katika eneo hilo Aprili 2019, ambapo lilikiri kuwa lilitekeleza mashambulio kwenye ngome za kijeshi karibu na mpaka wa Uganda.

IS katika propaganda zake hatahivyo haijawahi kutangaza wazi kuwa IS na ADF waliungana . Mwezi Septemba 2020, Baluku alitangaza kuwa kikundi cha ADF hakipo tena.

Alisema: "Sisi kwa sasa tuko jimbo, jimbo la Afrika ya kati, mojawapo ya maeneo yanayounda Islamic State ".

Hali ikoje katika DRC ? Kulingana na Shirika la wakimbizi la Umoaja wa Mataifa UNHCR kuanzia mwezi Januari 2021, ADF kimekwisha kuwauwa mamia ya raia wa nchi hiyo wasio na hatia na kuwafurusha makwao wengine zaidi ya 40.000 katika eneo la Beni.

Kundi hilo la wapiganaji limeshindwa kudhibitiwa na vikosi vya serikali ya DRC na vile vya Umoja wa Mataifa vya kulinda amani vilivyopo DRC -Monusco.

Tangia IS iiingie DRC, mashambulio ya mara kwa mara yalianza kuongezeka.

Mashambulio ya IS yamekuwa yakijitokeza katika maeneo yenye harakati za ADF kama vile Beni , Kivu kusini na wakati mwingine mashambulio hayo hufanyika katika jimbo la Ituri kweney mpaka na Kivu kusini

Chanzo: BBC