Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Algeria yavunja uhusiano na Morroco

Flags.png Algeria na Morroco

Thu, 26 Aug 2021 Chanzo: Channeltentanzania

Algeria imevunja rasmi mahusiano ya kidiplomasia na nchi jirani Morocco, huku waziri wake wa mambo ya kigeni akitaja msururu wa vitendo vya uhasama, Hatua hiyo inafikisha mwisho kipindi cha mvutano ulioongezeka kati ya nchi hizo za Afrika Kaskazini ambazo zimekuwa katika ugomvi wa miongo mingi, huku mipaka yao ikiwa imefungwa baina yao.

Morocco, kupitia wizara yake ya mambo ya nje, imesema inasikitishwa na uamuzi huo wa Algeria, ambao imesema hauna msingi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria Ramtane Lamamra amesema katika kikao cha waandishi wa habari kuwa miongoni mwa mambo mengine, Morocco imegeuza mipaka yake kuwa jukwaa la kuyaruhusu madola ya kigeni kutumia maneno ya kuichokoza Algeria.

Tangazo hilo limekuja karibu wiki moja baada ya Rais Abdelmadjid Tebboune kuuambia mkutano wa Baraza Kuu la Usalama la Algeria kuwa vitendo vya uhasama vinavyofanywa na Morocco vinamaanisha kuwa ipo haja ya kutathmini upya mahusiano kati ya nchi hizo.

Chanzo: Channeltentanzania