Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Algeria yasisitiza kuiunga mkono Palestina

Algeria Palestina Algeria yasisitiza kuiunga mkono Palestina

Mon, 16 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Salah Goudjil, Spika wa Baraza la Taifa la Algeria ambalo ndilo baraza la juu la bunge, alikutana na kiongozi wa ngazi za juu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas jana Jumapili na kusisitizia "uungaji mkono usioyumba" wa nchi yake kwa kadhia ya Palestina.

Katika mazungumzo yao hayo yaliyofanyika mjini Algiers, Goudjil na Sami Abu Zuhri, kiongozi mwandamizi wa Hamas anayeishi nje ya ardhi za Palestina, wamejadiliana jinai zinazoendelea kufanywa na utawala pandikizi wa Israel dhidi ya wananchi wa Ghaza zikiwemo njama za utawala huo dhalimu za kutaka kuwahamisha Wapalestina kaskazini mwa Ukanda wa Ghaza.

Spika wa Baraza la Taifa la Algeria ameitaka jamii ya kimataifa kuwalinda wananchi wa Palestina kwani hilo ni jukumu la jamii hiyo kwa mujibu wa sheria za kimataifa na kanuni za kibinadamu.

Katika mazungumzo hahyoi, Abu Zuhri ameishukuru Algeria kwa "uungaji mkono wake thabiti wa kadhia ya Palestina," na kusisitiza kuwa huo ndio msimamo unaopaswa kuchukuliwa na kila mwenye hisia za ubinadamu. Wananchi wa Morocco katika maandamano makubwa ya kulaani jinai za Israel huko Palestina

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) ilifanya mashambulizi ya kishjaa na kihistoria kwa kuwapiga Wazayuni kwa maelfu ya makombora na maroketi na kuingia katika ardhi za Palestina zilizopachikwa jina bandia la Israel, na kuteka baadhi ya kambi za kijeshi za Wazayuni na vitongoji kadhaa vya walowezi wa Kizayuni, Jumamosi ya wiki iliyopita ya tarehe 7 Oktoba, 2023. Baada ya kupata pigo hilo kubwa la kihistoria, Wazayuni wameamua kumalizia hamaki zao kwa wananchi wa kawaida, wanawake na watoto wadogo wa Palestina, jinai ambazo zinaendelea kulaaniwa kote ulimwenguni.

Watu wenye hasira kutoka na jinai hizo za Wazayuni wanaendelea kuandamana katika kona mbalimbali za duniani. Jana wananchi wa Morocco na Iraq na maeneo mengine ulimwenguni waliendeleza maandamano hayo ya kutangaza mshikamano wao na Wapalestina na kupinga jinai za Israel dhidi ya Ukanda wa Ghaza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live