Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Algeria yapeleka tani 150 za chakula Gaza

Mashambulizi Ya Angani Yaripotiwa Katika Mji Wa Rafah Huko Gaza Algeria yapeleka tani 150 za chakula Gaza

Mon, 25 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Hilali Nyekundu la Algeria jana Jumapili lilianza kupakia tani 150 za misaada ya kibinadamu kuelekea Ukanda wa Ghaza ambao unaelekea kutumbukia kwenye janga kubwa la njaa.

Shirika hilo limesema katika taarifa yake kwamba: "Msaada huo, unaobebwa na ndege nane za kijeshi, utaondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kijeshi wa Boufarik, ulioko umbali wa kilomita 30 kusini magharibi mwa mji mkuu Algiers, kuelekea Ukanda wa Ghaza huko Palestina kupitia Misri.

Msaada huo unatarajiwa kuwasili katika uwanja wa ndege wa Al Arish nchini Misri kabla ya kusafirishwa hadi Rafah kusini mwa Ghaza.

Utawala katili wa Israel umewafungia njia zote wakazi wa Ukanda wa Ghaza na hivi sasa maeneo yote ya ukanda huo hasa ya kaskazini yako katika hali mbaya ya ukosefu wa chakula na huduma zote muhimu na za dharura kwa mwanadamu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live