Waziri wa Mawasiliano wa Algeria amevishutumu vyombo vya habari vya Ufaransa kwa kuchochea mivutano, mizozo na ukosefu wa utulivu katika uhusiano wa nchi hiyo na Tunisia.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Tasnim, mwanaharakati mmoja wa Algeria ambaye alikuwa akitafutwa na Idara ya Mahakama ya nchi hiyo alivuka mpaka wa Algeria na Tunisia kinyume cha sheria wiki iliyopita na kukimbilia Ufaransa kupitia Tunisia.
Algeria ilimwita balozi wake kutoka Paris Jumatano iliyopita kulalamikia kushiriki wanadiplomasia wa Ufaransa katika tukio hilo. Ni kuwanzia wakati huo ndipo vita vya vyombo vya habari kati ya pande hizo mbili vilipozidi kupamba moto.
Waziri wa Mawasiliano wa Algeria amewaambia waandishi wa habari kwamba vyombo vya habari vya Ufaransa vimekuwa vikijaribu kushambulia taasisi za utawala za Algeria, ikiwa ni pamoja na taasisi ya rais na jeshi la taifa, kwa miaka mingi.