Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Algeria yaikosoa Ufaransa kwa kuingilia wimbo wake wa taifa

A376ED8B 68BF 47F9 986F 00DF480BCB0D.jpeg Algeria yaikosoa Ufaransa kwa kuingilia wimbo wake wa taifa

Mon, 26 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria ameijia juu Ufaransa kwa kujiingiza kwenye mjadala kuhusu wimbo wa taifa wa nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.

Ahmed Attaf, Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria amesema ameshangazwa na hatua ya Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Ufaransa ya 'kutoa maoni' kuhusu wimbo wa taifa wa nchi hiyo ya Kiarabu.

Catherine Colonna, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa amesema hatua ya Algeria ya kumshambulia mkoloni wake wa zamani kupitia wimbo wake wa taifa imepitwa na wakati.

Akijibu matamshi hayo, Ahmed Attaf, Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria amesema kwa kejeli kuwa, iwapo afisa huyo wa Paris anataka kujitosa kwenye mjadala huyo, basi yuko huru kutoa mwito wa kubadilishwa sauti na maghani ya wimbo huo iwapo hayamridhishi.

Hivi karibuni, Rais Abdelmajid Tebboune wa Algeria alipasisha dikrii ya kurejesha ubeti kogwe kwenye wimbo huo wa taifa, ambao unakosoa jinai za kikoloni za Ufaransa, na hata kumtaja mkoloni huyo kwa jina. Ubeti huo ulikuwepo katika wimbo wa taifa wa asili wa Algeria uliotungwa mwaka 1962.

Jinai za kikoloni za Ufaransa nchini Algeria Rais huyo amekuwa akisisitiza kuwa, wananchi wa Algeria hawatasahau jinai na uhalifu uliofanywa na Ufaransa huko humo. Amewahi kusema kuwa, ukoloni wa Ufaransa nchini kwake kuanzia mwaka 1830 hadi 1962 ulifanya uhalifu wa kutisha sana ambao haujashuhudiwa katika historia ya sasa ya mwanadamu.

Zaidi ya Waalgeria milioni moja waliuliwa na wanajeshi wa Ufaransa katika kipindi cha vita vya kupigania ukombozi wa Algeria kuanzia mwaka 1954 hadi 1962.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live