Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Algeria yaikatia waya Ufaransa kwenye hili…

Algeria Wayaaaa.jpeg Algeria yaikatia waya Ufaransa kwenye hili…

Wed, 31 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Algeria imemwita nyumbani balozi wake kutoka Ufaransa kupinga hatua ya serikali ya Paris kuingilia kati mpango wa Sahara Magharibi wa kuwa na mamlaka ya ndani.

Taarifa ya Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Ufaransa imeeleza kuwa, Algeria imeamua kuumuita nyumbano mara balozi wake kutoka Paris baada ya Ufaransa kutangaza kuunga mkono mpango wa Sahara Magharibi wa kuwa na Mamlaka ya Ndani.

Sehemu nyingine ya taarifa hiyo imeeleza kuwa, serikali ya Ufaransa imetangaza uungaji mkono wake wa moja kwa moja na wa wazi kwa jambo lililowekwa na kutwishwa na ukoloni katika eneo la Sahara Magharibi; hakuna hata serikali moja zilizotanguulia nchini Ufaransa iliyofanya jambo kama hilo, lakini serikali ya sasa imechukua uamuzi huu usio na tadibiri na bila kuzingatia matokeo yake.

Morocco ililitwaa eneo kubwa la Sahara Magharibi, koloni la zamani la Uhispania mwaka 1975 na tangu wakati huo imekuwa katika mzozo na mapigano na Harakati ya Polisario, inayoungwa mkono na Algeria, ambayo inapigania kuasisi nchi huru katika eneo hilo na kukomesha uwepo wa serikali ya Rabat.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live