Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Algeria yaendeleza rekodi ya kutofungwa

A.espncdn.com Algeria yaendeleza rekodi ya kutofungwa

Sat, 17 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

NCHI za Afrika zimekamilisha mitanange yake ya kujipima nguvu baada ya mechi kadhaa kuchezwa wiki hii.

Wakati mechi za klabu zikitarajia kuchezwa wikiendi ijayo, yafuatayo ni matokeo ya mechi hizo za kimataifa. ALGERIA 2-2 MEXICO Mabingwa watetezi wa Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) Algeria wameendeleza rekodi yao hya kutofungwa hadi kufikia mechi 20 baada ya kulazimishwa sare ya 2-2 dhidi ya mabingwa wa Kombe la Concacaf Gold Mexico licha ya kucheza karibu dakika zote wakiwa wachezaji 10.

Adlene Guedioura alitolewa nje dakika 10 baada ya mapumziko baada ya kupewa kadi ya pili ya njano. Algeria ilitoka nyuma baada ya Jesus Manuel Corona kuipatia Mexico bao katika dakika ya 43.

Mabingwa hao wa Afrika walifanya matokeo kuwa sawa dakika mbili baadae wakati kiungo Ismael Bennacer alipogimga kwa shuti hafifu akiwa ndani ya boksi.

Chanzo: habarileo.co.tz