Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Algeria na Uganda zasaini mikataba ya kuimarisha uchumi

Algeria Uganda Makubaliano Algeria na Uganda zasaini mikataba ya kuimarisha uchumi

Mon, 13 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Algeria na Uganda jana Jumapili zilitiliana saini mikataba kadhaa ya kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi baina yao. Hayo yamefanyika wakati wa ziara ya siku nne ya Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda mjini Algiers.

Shirika la habari la serikali la Algeria (APS) limeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, nchi hizo mbili zimetiliana saini hati mbili za maelewano katika masuala ya nishati pamoja na makubaliano mengine katika sekta za kilimo, utalii, na biashara.

Sherehe za utiaji saini mikataba hiyo zimefanyika katika ofisi ya rais kwenye mji mkuu wa Algeria, Algiers, na kuongozwa na Rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune na Rais Museveni.

Mapema hiyo jana, marais hao wawili walikutana kujadiliana masuala kadhaa yenye maslahi ya pamoja. Walijadiliana pia njia za kuratibu misimamo yao kwa shabaha ya kusaidia masuala mbalimbali yanayolihusu bara la Afrika na masuala ya kimataifa.

Tebboune amesema wakati wa mazungumzo yake hayo na Rais Museveni kwamba wafanyabiashara 150 wa Algeria wataelekea Kampala, mji mkuu wa Uganda kwa ajili ya kufuatilia utekelezaji wa mikataba hiyo na kujadili uwezekano wa ushirikiano baina yao na makampuni ya Uganda, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuimarisha uhusiano wa nchi hizo mbili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live