Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Algeria mwenyeji mkutano wa kuishitaki Israel ICC

Israel Haina Mpango Wa Kuteka, Kukalia Au Kuitawala Gaza   Netanyahu Algeria mwenyeji mkutano wa kuishitaki Israel ICC

Tue, 28 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Algeria imejiunga na orodha ya nchi zinazotaka kufanyike uchunguzi kuhusiana na jinai za kivita zilizofanywa na Israel katika Ukanda wa Gaza, na kushtakiwa utawala haramu katika vyombo vya kimataifa.

Tayari Karim Khan, Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC amepokea maombi kutoka kwa nchi tano (Afrika Kusini, Bangladesh, Bolivia, Comoro na Djibouti) ya kutakiwa kuchunguza jinai za utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza.

Shirika la habari la IRNA limemnukuu Ibrahim Tairi, Mkuu wa Chama cha Taifa cha Mawakili Algeria akisema nchi hiyo itakuwa mwenyeji wa mkutano wa kujadili njia za kuuchunguza na kuushtakia utawala wa Kizayuni ICC na katika mahakama nyingine za kimataifa.

Tairi amesema mkutano huo wa kimataifa wa siku mbili utakaoanza kesho Novemba 29, utawaleta pamoja wataalamu wa sheria kutoka nchi mbalimbali za Kiarabu na Ulaya.

Kabla ya hapo, Rais wa Algeria alitoa mwito wa kushtakiwa Israel ICC na kusisitiza kwamba, utawala ghasibu haujali wala kuheshimu maamuzi ya taasisi muhimu za kimataifa kama Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live