Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Algeria imechukua tahadhari kudhibiti msambao wa kunguni

Hofu Ya Uvamizi Wa Kunguni Yaongezeka Kabla Ya Olimpiki Ya 2024 Algeria imechukua tahadhari kudhibiti msambao wa kunguni

Fri, 6 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka nchini Algeria imeimarisha hatua za afya katika mipaka yake ili kupunguza kuenea kwa kunguni, ambao wameenea kote Ufaransa.

Wizara ya afya katika nchi hiyo ya Afrika Kaskazini ilisema kuwa inaanzisha ufuatiliaji wa afya na kuua vijidudu kwa ndege, meli na magari katika sehemu za kuingilia.

Hii inakuja huku kukiwa na wasiwasi kwamba wadudu hao wanaonyonya damu wanaweza kuingia Algeria kutokana na idadi kubwa ya watu wanaosafiri kutoka Ufaransa.

Hata hivyo wizara hiyo imesema hakuna uvamizi wa kunguni ambao umeripotiwa nchini huku ikisisitiza kuwa makini.

Nchi jirani ya Morocco nayo pia tayari imetangaza mikakati ya kuzuia msambao wa wadudu hao katika eneo lake.

Masambao wa kunguni jijini Paris na miji mingine imezua wasiwasi nchini Ufaransa kuelekea mashindano ya Olimpki mwaka ujao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live