Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Alaaa! Atwoli asema huenda kiti cha COTU ni chake milele

0fgjhs45o2a7k76q1 Alaaa! Atwoli asema huenda kiti cha COTU ni chake milele

Mon, 12 Apr 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Francis Atwoli amesema huenda muhula wake wa mwisho kama Katibu Mkuu wa COTU hautaisha

- Atwoli alichaguliwa tena kuongoza muungano huo kwa miaka mingine mitano Ijumaa, Aprili 9

- Hata hivyo, mnamo Januari 2021, Atwoli alisema alikuwa anajiandaa kustaafu

Katibu Mkuu wa Muungano wa vyama vya kutetea haki za wafanyakazi (COTU) Francis Atwoli amesema huenda hatawahi kustaafu kutoka kwa wadhifa huo.

Atwoli alisema haya baada ya kuchaguliwa bila kupingwa kwa muhula wa tano kama katibu mkuu wa COTU, wadhifa ambao amekuwa akishikilia tangu mwaka 2001.

Akizungumza Jumapili, Aprili 11, Atwoli alisema huenda hatawahi kustaafu tena.

"Kama mambo yalivyo, huenda sitawahi kuwa na muhula wa mwisho katika wadhifa huu. Naweza kuwa hapa kwa muda ilhali wanaoniamini na usalama wa kazi zao wananitaka," alisema.

Mtetezi huyo wa haki za wafanyakazi amekuwa akishikilia wadhifa huo tangu mwaka 2001 akimrithi Joseph Mugalla.

Hata hivyo, mnamo Januari 2021, Atwoli alisema alikuwa anajiandaa kustaafu.

"Napunga hewa katika shamba langu ndogo la Nakuru nawachunga ngo'mbe wangu na chakula kinaandaliwa msimu wa ukame, nikijiandaa kustaafu," alisema Januari 14, 2021.

Sasa atahudumu kwa muhula wa miaka mitano baada ya wajumbe wa COTU kumchagua kwa wingi mpinzani wake ambaye ni Katibu Mkuu wa Chama cha Kitaifa cha Wauguzi (KNUN) Seth Panyako alipojiondoa.

Baada ya kuchaguliwa kwake, Atwoli aliwashukuru Wakenya wote kwa kumpigia kura.

“Nataka kuwashukuru Wakenya wote kwa kunichagua bila kupingwa, kupitia vyama vyao, kama katibu mkuu wa @COTU_K. Ninaahidi kuwahudumia na nguvu zangu zote na bila kuwasaliti," Atwoli aliandika kwenye Twitter.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke