Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Al-shabab 60 wauawa na vikosi vya usalama Kenya

Kenya Alshabaab Kuuawa Al-shabab 60 wauawa na vikosi vya usalama Kenya

Fri, 4 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vikosi vya usalama vya Kenya vimewauwa karibu wapiganaji 60 wa kundi la kigaidi la al-Shabab la Somalia.

Waziri wa Usalama wa ndani wa Kenya Kithure Kindiki amesema kuwa, askari wa Kenya walikabiliana na wanamgambo hao kaskazini mashariki mwa Kenya katika eneo la Tana River.

Waziri huyo aidha amesema kuwa, wapiganaji hao waliyalenga mabasi ya abiria, lakini vikosi vya usalama vilivyokuwa vimeshika doria vilijibu haraka shambulizi hilo na kuwauwa wanamgambo wote.

Taarifa zaidi zinasema kuwa, raia wawili waliuawa katika shambulizi hilo.

Kumekuwa na mashambulizi ya mara kwa mara kaskazini mwa Kenya ya kundi la al-Shabab ambalo linaendesha harakati zake katika nchi jirani Somalia. Wanachama wa kundi la kigaidi la al-Shabab

Mapema Julai, vikosi vya usalama vya Kenya viliwauwa wapiganaji 20 wa kundi hilo katika shambulizi sawa na hilo.

Ikumbukwe kuwa, shambulio la kigaidi katika Chuo Kikuu cha Garissa mwaka 2015, ni shambulio kubwa zaidi kuwahi kufanywa nchini Kenya tangu mwaka 1998. Watu 148 waliuawa, wengi wao wakiwa wanafunzi wa chuo hicho katika shambulio hilo la kivamizi la al-Shabab.

Kundi la kigaidi la al-Shabab ni tawi la mtandao wa kigaidi al-Qaeda nchini Somalia na limefanya mashambulizi kadhaa ya kigaidi nchini Kenya likilenga idara za serikali, askari, magari ya abiria na mahoteli.

Kundi hilo la kigaidi limekuwa likifanya kila liwezalo kuipindua serikali kuu ya Somalia tangu mwaka 2007; na hadi sasa limefanya mashambulizi mengi ya kigaidi na kuuwa wanajeshi na raia wengi huko Somalia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live