Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Al-Shabab washambulia hoteli katika mji mkuu wa Somalia

Al Shabab Washambulia Hoteli Katika Mji Mkuu Wa Somalia Al-Shabab washambulia hoteli katika mji mkuu wa Somalia

Fri, 15 Mar 2024 Chanzo: Bbc

Wanamgambo wa kundi la al-Shabab wameshambulia hoteli moja karibu na ikulu ya rais katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu, vyanzo vya usalama na mashahidi wanasema.

Kundi hilo limewahi kushambulia hoteli ya Syl ambayo ni maarufu kwa maafisa wa serikali.

Walioshuhudia waliripoti milipuko na milio ya risasi kutoka katika hoteli hiyo, wakiambia Reuters kwamba wapiganaji walikuwa bado wako ndani.

Haikuweza kubainika mara moja iwapo kulikuwa na majeruhi.

"Mujahideen wenye silaha wanadhibiti hoteli hiyo na wanawapiga risasi wafanyakazi na maafisa" wa serikali katika hoteli hiyo, al-Shabab walisema katika taarifa wakidai kuhusika na shambulio hilo.

Mkazi Farah Ali, ambaye anaishi karibu na ofisi ya rais, aliiambia Reuters: " Kwanza tulisikia mlipuko mkubwa, na kisha milio ya risasi ikafuata. Tunafahamu kwamba wapiganaji wako ndani ya [hoteli] kwa sababu tunasikia wakifyatuliana risasi."

"Wapiganaji kadhaa waliingia ndani ya jengo hilo kwa nguvu baada ya kuharibu ukuta wa pembezoni kwa mlipuko mkubwa," afisa wa usalama aliambia AFP.Hassan Nur, ambaye alitoroka kwa kupanda ukuta na kuruka upande wa pili, alisema: "Sijui kuhusu majeruhi lakini kulikuwa na watu wengi ndani wakati shambulio hilo lilipoanza."

Mashahuda wengine waliripoti kuona polisi wakiwasili ndani ya dakika chache baada ya shambulio hilo, ambalo lilisababisha makabiliano ya risasi na wanamgambo.

Mashambulizi yamepungua katika wiki za hivi karibuni huku usalama kuimarishwa baada ya serikali kuzidisha mashambulizi yake ya kijeshi dhidi ya kundi hilo.

Al-Shabab inadhibiti maeneo makubwa ya kusini na katikati mwa Somalia.

Chanzo: Bbc