Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Al-Qaeda yatangaza kifo cha waliyemshika mateka raia wa Mali

Mali Alqaeda Al-Qaeda yatangaza kifo cha waliyemshika mateka raia wa Mali

Fri, 13 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kundi la Al-Qaeda tawi la Afrika Magharibi limetangaza kifo cha waliyemshika mateka raia wa Mali akiwa chini ya ulinzi wake, na kumtaja kwa jina la Idriss Sanogo na kusema alifariki kutokana na ugonjwa ambao haukutajwa.

Kundi la Jamaat Nusrat al-Islam wal-Muslimin (JNIM) lilituma salamu za rambirambi kwa familia ya mwanamume huyo.

JNIM pia ililaumu serikali ya Mali, ikisema imeshindwa kujadili kuachiliwa kwa Bw. Sanogo.

Kundi hilo lilitangaza habari hiyo katika taarifa fupi siku ya Alhamisi kupitia mitandao ya kijamii.

Ilitoa taarifa kidogo kuhusu Bw Sanogo, mbali na kusema alizaliwa mwaka wa 1952 na alitekwa nyara na wanamgambo wa JNIM katika mji wa Timbuktu nchini Mali miaka mitatu iliyopita.

Mapema Mei 2020, vyombo vichache vya habari viliripoti kutekwa nyara kwa afisa huyo wa serikali - katika eneo la Timbuktu - akimtaja kama "Drissa Sanogo" na "Idrissa Sonogo".

Hadi Alhamisi, JNIM haikuwa imetaja hadharani kuwa inamshikilia Bw Sanogo.

Katika taarifa yake ya hivi punde zaidi, kundi la al-Qaeda lilisema serikali "inawajibika kikamilifu" kwa kifo cha Bw Sanogo, likisema Bamako "alipuuza kesi yake... licha ya kujua hali ya afya yake".

Kundi hilo la wanamgambo lilisema mahitaji yake ni "rahisi" na "yanajulikana kwa wote": "mkomboe ndugu yetu, tunamwachilia ndugu yako" - na kupendekeza kwamba kundi la wanajihadi limetaka kuachiliwa kwa mmoja au wanamgambo wake kadhaa kwa mabadilishano na Bwana Sanogo.

Serikali ya Mali bado haijajibu lolote kutokana na kauli ya JNIM.

Taasisi inayolenga Afrika ya Mafunzo ya Usalama (ISS) ilisema katika ripoti ya hivi majuzi kwamba utekaji nyara wa watu wa ndani nchini Mali na Burkina Faso umeongezeka, na kuishutumu JNIM kwa kuwa mhusika mkuu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live