Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Al-Qaeda yashtumu jeshi kwa kufanya 'mauaji' dhidi ya raia Burkina Faso

Al Qaeda Yashtumu Jeshi Kwa Kufanya 'mauaji' Dhidi Ya Raia Burkina Faso Al-Qaeda yashtumu jeshi kwa kufanya 'mauaji' dhidi ya raia Burkina Faso

Thu, 29 Feb 2024 Chanzo: Bbc

Tawi la Al-Qaeda la Sahel limeshutumu jeshi la Burkina Faso kwa kufanya "mauaji" dhidi ya raia kaskazini mwa nchi hiyo.

Kundi hilo linadai jeshi la serikali liliwau watu 223 tarehe 25 Februari baada ya "kushindwa kuzima" shambulio la kijihadi.

Jamaat Nusrat al-Islam wal-Muslimin (JNIM) ilitoa shutuma hizo kupitia taarifa iliyochapishwa kupitia matandao wake wa Telegram ikisema ''uhalifu wa jeshi la Burkina Faso dhidi ya watu unaendelea".

Kundi hilo pia lilitoa picha kuthibitisha madai ya ukatili dhidi ya raia.

JNIM ilisema kuwa mnamo tarehe 25 Februari, vikosi vya Burkina Faso vilitekeleza "mauaji ya kutisha dhidi ya raia wasio na silaha" kati ya mji wa Ouahigouya na eneo linalotafsiriwa kwa Kiarabu kama "Tio", ambalo huenda linamaanisha mji wa karibu wa Titao.

Waathirika wa mashambulizi yanayodaiwa kufanywa na jeshi ''wengi wao wakiwa wanawake na watoto", kulingana na taarifa hiyo.

Chanzo: Bbc