Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Al Ahly yamkosha Mascherano

0877c1852ca8f534cdaee77aaf2d279c.png Al Ahly yamkosha Mascherano

Fri, 12 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

WANASOKA wa zamani wa Amerika ya Kusini, Javier Mascherano na Julio Cesar wamevutiwa na kiwango kilichoonyeshwa na Al Ahly ya Misri kwenye michuano ya kombe la dunia ngazi ya klabu.

Wakongwe hao walisema licha ya kupoteza kwa mabao 2-0 dhidi ya mabingwa wa Ulaya, Bayern Munich kwenye usu fainali juzi, kiwango cha Al Ahly kimeonyesha mabadiliko makubwa katika soka la Misri.

Mascherano ambaye mecheza mechi 147 kwa Argentina na kipa wa Brazil Cesar walizungumza hayo saa chache kabla ya mechi ya kuwania nafasi ya tatu kati ya Al Ahy na mshindi wa Copa Libertadores Brazil Palmeiras iliyotarajiwa kuchezwa jana.

"Wameacha fikra chanya (Al Ahly kwenye mechi ya nusu fainali dhidi ya Bayern Munich) kwamba soka ya Misri imekuwa juu kwa miaka ya karibuni,” alisema mchezaji wa zamani wa Liverpool na Barcelona Mascherano.

"Na pia jinsi mchezaji wa kiwango cha dunia kama Mohamed Salah alivyopeleka soka ya Misri kwenye kiwango kingine.”

"Ukiitizama Al Ahly unaona kwamba Salah hayuko peke yake, lakini mbali na hilo linapokuja suala la kuendeleza wachezaji na kuwa wenye ushindani, Misri wako vizuri na watafanya vizuri zaidi miaka ijayo.”

Cesar aliyeichezea Brazil mechi 87 na kushinda mataji matano ya Serie A akiwa na Inter Milan, naye alivutiwa na kile alichokiona kwa mabingwa hao mara tisa wa Afrika.

"Tuliona timu iliyocheza dhidi ya Bayern Munich ikitengeneza nafasi na kushambulia.”

"Bayern Munich ni moja ya timu bora duniani na labda ndio bora kwa sasa, unaweza kuwa na hakika pia kwamba Palmeiras itafanya jitihada kujaribu kushinda nafasi ya tatu.”

"Kuna siku nilikuwa na Kaka tukafurahia timu za Misri. Tulipata nafasi ya kucheza dhidi ya Misri mwaka 2009 kwenye Kombe la Shirikisho la Fifa (Brazil ilishinda 4-3, shukrani kwa bao la dakika za mwisho, lakini tulishangazwa na uwezo walioonyesha.”

Chanzo: habarileo.co.tz