Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Akutwa mochwari akiwa hai dakika 120

Constance Glantz Sd Akutwa mochwari akiwa hai dakika 120

Wed, 5 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamke mmoja katika Jimbo la Nebraska nchini Marekani amekuwa gumzo katika Vyombo vya habari baada ya kukutwa yupo hai katika chumba cha kuhifadhia maiti (Mochwari), ikiwa ni muda mfupi toka Wauguzi katika nyumba za kutunza Wazee wamtangaze kuwa amefariki dunia.

Mwanamke huyo aitwae Constance Glantz (74), alikutwa anapumua baada ya Wafanyakazi katika chumba cha kuhifadhia maiti kuanza mchakato wa kuandaa kile walichofikiria kuwa ni maiti ikiwa ni saa mbili zimepita toka Wafanyakazi katika nyumba ya kuhifadhi Wazee kutangaza kifo cha Bibi huyo.

Familia ya Glantz ilifahamishwa kuhusu kilichotokea na tayari Polisi wameanza uchunguzi na kutembelea Makazi ya Waverly wanakolelewa Wazee.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live