Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Akiri kuvuta bangi kumuunga mkono mgombea Urais

Bangi Akiri Mkir=gombea Akiri kuvuta bangi kumuunga mkono mgombea Urais

Thu, 14 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanaume mmoja nchini Kenya Boniface Mutua mwenye miaka 47, ameishangaza mahakama ya Eldoret baada ya kukiri kuvuta bangi na kusema anafanya hivyo kumuunga mkono mgombea Urais nchini humo Prof. George Wajackoyah.

George amekuwa kivutio nchini Kenya hasa kwa sera yake anayosisitiza kuhalalisha kilimo cha bangi kwa ajili ya kukuza uchumi

Mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Christine Menya, mtuhumiwa huyo alidai anatumia bangi kama kichocheo, na kumuunga mkono mgombea urais anayempenda Prof. George Wajackoyah.

Mutua ambaye alikiri mashtaka yanayomkabili, alidai kuwa bangi inamsukuma kuwa na  ujasiri na nguvu ya kumfanyia kampeni Wajackoyah.

Mutua alikamatwa katika shamba la Bahati huko Ainabkoi, kaunti ya Uasin Gishu, baada ya kupatikana na roli tatu za bangi zote zenye thamani ya sh90 za Kenya

Hakimu alilisisitiza kuwa ni kinyume cha sheria za Kenya kumiliki au kuvuta bangi nchini Kenya hivyo mtuhumiwa ana kesi ya kujibu. Kesi hiyo itaendelea Julai 27, 2022.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live