Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Akatwa Korodani na Mkewe Kisa Hamridhishi Kitandani

Mgonjwazz.jpeg Akatwa korodani

Sun, 21 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MEME Kabati ambaye ni Raia wa Kenya mwenye umri wa miaka 56 amelazwa katika Hospitali ya Nyambene Kaunti ya Meru baada ya Mkewe Karambu Meme, kumvuta na kuikata korodani yake moja kwa madai ya kwamba korodani hizo hazina faida kwasababu mumewe hajawahi kumridhisha kimapenzi kitandani hata siku moja wakati wanapofanya tendo la ndoa.

Tukio hilo limetokea wakiwa nyumbani kwao Igembe, Chifu wa eneo hilo la Ntunene aitwaye Edward Mutalii amesema alipata taarifa na alipofika eneo la tukio alikuta korodani ya mwanaume huyo ikiwa chini baada ya kuvutwa sana mfuko wa uzazi na Mkewe na kuikata korodani moja.

Polisi wamemkamata mwanamke huyo na kwa sasa anashikiliwa akisubiri kufikishwa mahakamani lakini Mwanamke huyo anasisitiza amefanya hivyo kwakuwa kamwe mumewe hajawahi kumridhisha wakati wa kufanya tendo la ndoa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live