Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Akamatwa mochwari akiharibu miili ya marehemu

11525278 16x9 940x529 Akamatwa mochwari akiharibu miili ya marehemu

Mon, 2 Nov 2020 Chanzo: millardayo.com

Mhudumu wa zamani wa chumba cha kuhifadhai maiti  ya Hospitali ya Rufaa ya Iten, Kaunti ya Elgeyo-Marakwet nchini Kenya amekamatwa na maafisa wa polisi kwa tuhuma za kuharibu miili iliyohifadhiwa hospitalini humo.Benson Kagari ambaye ni mhudumu wa zamani wa mochwari hiyo, anaripotiwa kuingia katika mochwari ya hospitali hiyo Jumatano, Oktoba 28,2020 usiku, bila kugunduliwa na mtu yeyote.Kwa mujibu wa taarifa ya gazeti la Taifa leo, Waziri wa Afya katika Jimbo hilo, Isaac Kamar amesema mshukiwa aliingia katika hifadhi hiyo kupitia kwa dirisha na kuelekea hadi eneo ambapo miili hiyo ilikuwa imehifadhiwa. Inadaiwa mshukiwa alikuwa akiingia hospitalini humo kuharibu miiili iliyokuwa imehifadhiwa, Kamar amesema mshukiwa alitimuliwa hospitalini humo kutokana na utovu wa nidhamu.  “Tulipokea ripoti kwamba kulikuwa na mtu aliyeingia kwenye mochari ambapo alikuwa akiharibu miili iliyohifadhiwa na kuibadilisha ili kuwachanganya wahudumu.Tulifika kwa haraka na kubaini kuwa ni mhudumu wa zamani aliyefutwa kazi kutokana na utovu wa nidhamu” KamarKulingana na Kamar, baada ya kupokea ripoti hiyo maafisa wa afya waliingia chumbani humo kwa haraka na kumfumania mshukiwa ambapo walimkamata na baadaye walimkabidhi kwa polisi ili kuchunguzwa. Inasemekana kuwa mshukiwa alitumiwa na baadhi ya watu flani kuwaharibia jina wafanyakazi katika hospitali hiyo ili kuonekana watepetevu.UWEZO WA MAKOMANDO WA JWTZ, UTABAKI MDOMO WAZI

Chanzo: millardayo.com