Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ajificha kwenye tairi la ndege kutoka Algeria hadi Ufaransa

Marekani Inafikiria Jinsi Ya Kuboresha Ndege Zisizo Na Rubani Ili Kuzipeleka Ukraine Ajificha kwenye tairi la ndege kutoka Algeria hadi Ufaransa

Fri, 29 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 20, amekutwa akiwa hai baada ya kujificha kwenye sehemu ya matairi ya ndege iliyosafiri kutoka Algeria hadi Ufaransa.

Mtandao wa DW Kiswahili umeripoti kuwa Kijana huyo aligunduliwa na Wakaguzi wa ndege akiwa katika hali mbaya kiafya na baadaye aliwahishwa Hospitalini.

Ndege hiyo ya abiria ilitokea Mji wa Oran na kutua jana katika uwanja wa ndege wa Orly mjini Paris, kwa mujibu wa takwimu za Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Marekani (FAA), Watu 132 walijaribu kusafiri kwa kutumia mfumo huo kati ya mwaka 1947 na 2001.

Kwa kawaida, ndege hizo za abiria hupaa angani hadi kwa urefu wa futi 30,000 hadi 40,000 ambapo nyuzijoto hushuka mno hadi kufikia karibu chini ya 50 kipimo cha Celsius na hivyo kuwa hatari kwa Mtu anayesafiri katika eneo la matairi kukosa hewa na kukabiliwa na baridi kali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live