Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ajali za barabarani zinavyomaliza watu Nigeria

Ajali Ajaliiiii Nigeria Tinubu Ajali za barabarani zinavyomaliza watu Nigeria

Wed, 10 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ajali za barabarani zimendelea kuchukua roho za watu nchini Nigeria ambapo katika ajali ya karibuni kabisa iliyoripotiwa ni ile iliyotokea jana Jumatatu na kuua watu 10. Ajali hiyo imehusisha lori na basi yaliyogongana karibu na kijiji cha jimbo la Kwara kaskazini mwa Nigeria.

Stephen Dawulung, Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani cha Serikali ya Shirikisho la Nigeria huko Kwara, akiwaambia hayo waandishi wa habari na kuongeza kuwa, kwa uchache watu 10 wamefariki dunia na wengine kadhaa wamejeruhiwa kwenye ajali hiyo iliyotokea kwenye barabara ya Moro ya na kijiji hicho cha Kwara cha kaskazini mwa Nigeria.

Tukio hilo lilitokea kutokana na uendeshaji mbaya wa lori na kusababisha kugongana uso kwa uso na basi lililokuwa linalokuja upande wa pili na kuongeza kuwa, watu hao 10 wamefariki dunia papo hapo.

Dawulung ametoa onyo kali kwa madereva wasioheshimu sheria na wanaoendesha magari kwa kasi kupita kiasi.

Katika upande mwingine, rais wa Nigeria, Bola Tinubu amemsimamisha kazi Betta Edu, waziri wa masuala ya kibinadamu na kukabiliana na umaskini kutokana na mgogoro uliozuka hivi karibuni kwenye ofisi yake.

Inadaiwa kuwa, waziri huyo alimwandikia barua mhasibu mkuu wa Nigeria mwishoni mwa Diesemba 2023, kuamuru kutiliwa kiasi kikubwa cha fedha katika hesabu yake ya benki.

Kutokana na hali kuwa hivyo, Tinubu amemuamrisha waziri huyo aliyesimamishwa kazi kukabidhi kazi zake mara moja kwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo na atoe ushirikiano kamili kwa mamlaka husika zinazhofanya uchunguzi kuhusu kesi yake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live