Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ajali yaua wwtu 45, mtoto anusurika

Ajali 0 WA0002 Ajali yaua wwtu 45, mtoto anusurika

Sat, 30 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu 45 wamepoteza maisha nchini Afrika Kusini baada ya basi walilokuwa wanasafiria kutumbukia kwenye korongo na kuwaka moto.

Ajali hiyo ilitokea juzi Alhamisi ambapo mtoto wa miaka minane pekee ndiye aliyenusurika katika ajali hiyo na alipelekwa hospitali akiwa na majeraha mabaya. Wizara ya uchukuzi ya nchini humo ilisema kuwa basi hilo lilikuwa linaelekea Moria kaskazini mwa nchi hiyo likitokea nchi jirani ya Botswana.

Ilielezwa kuwa dereva alishindwa kudhibiti gari na kugongana vizuizi vya daraja kisha kupita juu ya daraja na kufika chini ambapo liliwaka moto.

Operesheni za uokoaji ziliendelea hadi nyakati za jioni huku baadhi ya miili ikiwa imeungua kiasi cha kushindwa kutambulika na mingine ikiwa imekwama ndani ya mabaki ya basi na uraia wa abiria ulikuwa unakaguliwa bado.

Una maoni, tuandikie.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live