Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ajali ya boti DRC 200 watafutwa

01a32231cd10e8c544ee220a8d4e736a.png Ajali ya boti DRC 200 watafutwa

Thu, 18 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

Baada ya Waziri wa Maswala ya Kijamii na Ubinadamu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Steve Mbikayi kuthibitisha kuokoa watu 300 kufuatia ajali ya boti iliyotokea juzi na kuua watu 60, imeelezwa kuwa utafiti unaendelea kutambua ilipo miili mingine ya watu 200 waliopotea kutokana na ajali hiyo.

Boti hiyo ilizama jumatatu katika mto mmoja uliopo mkoa wa Mai Ndombe Magharibi mwa nchi hiyo ambapo waziri huyo alitbitisha kuwa vikosi vya uokoaji kuendelea na zoezi la kuopoa baadhi ya miili ya watu.

Kwa mujibu wa Mbikayi, zaidi ya watu 700 walikuwa katika boti hiyo huku ikiwa haijafahamika kama watu hao 200 wamefariki au wapo hai, licha ya zoezi la kuwatafuta likiwa linaendelea kwa siku ya tatu mfululizo.

Chanzo: habarileo.co.tz