Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ajali ya basi nchini Afrika Kusini yaua takriban watu 20

Ajali Gari Afrika Kusini Ajali ya basi nchini Afrika Kusini yaua takriban watu 20

Mon, 18 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vyombo vya habari vya ndani ya Afrika Kusini vimeripoti kuwa takriban watu 20 wamepoteza maisha baada ya lori lilipogongana na basi lililokuwa likisafirisha wachimba migodi katika jimbo la Limpopo la kaskazini mwa nchi hiyo.

Tovuti ya Times Live imeinukuu kampuni ya ulinzi ya eneo hilo, iitwayo Arezwothe Protection Services ikisema kwamba, abiria wengi waliokuwemo kwenye basi hilo walifariki katika eneo la ajali.

Kampuni hiyo ya ulinzi imesema kuwa, ajali hiyo ilitokea mwendo wa saa kumi na moja jioni katika eneo lililoko kati ya Niani na Musina, umbali wa kilomita chache kutoka mpaka wa Afrika Kusini na Zimbabwe.

Toleo la mtandaoni la jarida la SA Trucker linalojishughulisha na taarifa za madereva wa malori wa kusini mwa Afrika, limesema kwamba, basi na lori hilo yaliwaka moto baada ya kugongana huku huku abiria wakiwa bado wamenasa ndani ya basi hilo.

Kwa mujibu wa taarifa ya gazeti la Arezwothe Protection Services iliyotumwa kwenye mtandao wa kijamii wa X yaani ambazo zamani ulikuwa unaitwa Twitter, magari hayo yamegongana wakati moja lilipokuwa likisafirisha wachimba migodi kuwapeleka kwenye Mgodi wa almasi wa Venetia.

Mgodi wa Venetia, unaomilikiwa na De Beers, ndiye mzalishaji mkubwa zaidi wa almasi nchini Afrika Kusini.

Hadi wakati inaripotiwa habari hii, maafisa wa mkoa wa Limpopo hawakupatikana kuweza kutoa ufafanuzi na maelezo yao kuhusu ajali hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live