Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ajali ya basi na lori yaua 48

FB IMG 1688217002765 Ajali ya basi na lori yaua 48

Sat, 1 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Takriban watu 48 wamethibitishwa kufariki na wengine kadhaa kulazwa hospitalini katika Kaunti ya Kericho kufuatia ajali mbaya iliyotokea katika barabara ya makutano ya Londiani Ijumaa jioni.

Waziri wa Uchukuzi wa Kenya Kipchumba Murkomen alipotembelea aneo la tukio la ajali, amesema kuwa lori lililohusika katika ajali hiyo halikuwa la ndani ya Kenya kwani lilikuwa na nambari ya usajiri ya Rwanda.

Ajali hiyo ya iliyotokea majira ya saa kumi na mbili unusu jioni ilitokea baada ya lori kupoteza mwelekeo, na kuwagonga wapiti njia, wafanyabiashara na mabasi ya abiria al maarufu matatu yaliyokuwa kando ya barabara.

Lori hilo liliyagonga mabasi manne, lori mbili, gari la kibinafsi na basi lingine kubwa la abiria.

Lori hilo lilikuwa likielekea Kericho kabla ya kushindwa kuacha njia, na kuwagonga makumi ya wachuuzi waliokuwa wakiendelea na shughuli mbali mbali kando ya barabara kuu ya Nakuru-Kericho.

Waziri wa Barabara Kipchumba Murkomen alitembelea eneo hilo Jumamosi asubuhi, akiandamana na maafisa wengine.

Alisema juhudi za uokoaji zinaendelea zikihusisha maafisa kutoka mashirika mbalimbali ya serikali ya kitaifa na kaunti.

"Juhudi za uokoaji zitafuatiwa na uchunguzi kubaini chanzo cha ajali hiyo," aliongeza.

Walioshuhudia ajali hiyo walisema, dereva wa lori hilo alikuwa akijaribu kukwepa kuligonga basi lililokuwa limeegeshwa barabarani baada ya kuwa na kasoro ya kimitambo kabla ya kushindwa kulimudu.

Zaidi ya watu 60 kufikia sasa wamekimbizwa katika hospitali tofauti za Londiani, Kericho na Nakuru ambako wanapokea matibabu kwa sasa.

Jana jioni, juhudi za uokoaji zilikwama kutokana na mvua kubwa iliyoshuhudiwa katika eneo la tukio.

Rais William Ruto aliongoza taifa kuomboleza vifo hivyo.

Akitumia Twitter Ijumaa usiku, alitweet, "Nchi inaomboleza pamoja na familia ambazo zimepoteza wapendwa wao katika ajali mbaya ya barabarani eneo la Londiani, Kaunti ya Kericho. Inasikitisha kwamba baadhi ya walioaga dunia ni vijana wenye mustakabali mzuri na biashara. watu ambao walikuwa kwenye kazi zao za kila siku." Aliendelea, "Tunawaombea wapone haraka wote walionusurika; mko kwenye mawazo yetu. Tunawaomba madereva wa magari kuwa waangalifu sana barabarani, hasa wakati huu tunapokabiliwa na mvua kubwa."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live