Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ajali ya Boti yauwa 26, wengine hawajulikani walipo

Mweh Ajali Maji Ajali ya Boti yauwa 26, wengine hawajulikani walipo

Mon, 11 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Takriban watu 26 wamekufa na wengine kadhaa hawajulikani walipo kufuatia ya ajali ya boti iliyotekea Septemba 10, 2023 katika eneo la Mokwa lililopo kaskazini mwa Nchi ya Nigeria.

Kwa mujibu wa Msemaji wa Gavana wa Jimbo la Niger, Bologi Ibrahim amesema boti hiyo ilikuwa na watu zaidi ya 100, wakiwemo wanawake na watoto na ilipata ajali kutokana na kubeba watu wengi kupita kiasi na uchakavu wa usafiri huo.

Aidha, Viongozi wa eneo hilo pia wamesema watu wengine 30 wameokolewa, huku wakibainisha kuwa ajali hiyo ni mbaya zaidi kushuhudiwa jimboni humo katika kipindi cha miezi mitatu.

Mapema mwezi Julai 2023, zaidi ya watu 100 walikufa wakati mashua iliyojaa kupita kiasi iliyopinduka katika jimbo la Niger, ikiwa ni mojawapo ya ajali kubwa zaidi katika miaka ya hivi karibuni nchini humo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live