Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ahukumiwa kifungo Tunisia kwa kosa la kukejeli aya ya Kuran

Emna Charqui Emna Charqui

Wed, 15 Jul 2020 Chanzo: BBC

Mwana blogu nchini Tunisia amehukumiwa kifungo cha miezi sita gerezani baada ya kuchapisha taarifa kuhusu Covid-19 ikiwa imeandikwa kwa mtindo wa aya kutoka kwenye kitabu kitakatifu cha Koran.

Emna Charqui,28, alikamatwa mwezi Mei kwa kuchapisha ujumbe kwenye ukurasa wa Facebook akiwataka watu kufuata sheria za usafi kwa kuigiza namna ambavyo kitabu hicho kitakatifu kinaeleza.

Charqui alisema kwenye mahojiano ya hivi karibuni kuwa hakuwa na nia ya kusababisha taharuki, lakini aliona kuwa ujumbe huo unafurahisha.

Alikutwa na hatia katika mahakama ya mjini Tunis kwa kosa la ''kuchochea chuki miongoni mwa watu wa dini tofauti.''

Charqui ana mpango wa kukata rufaa. Tarehe 2 mwezi Mei, Charqui aliweka kwenye mtandao wa kijamii ujumbe akiigiza aya kutoka kwenye Koran.

Kwenye maandishi aliwataka watu kunawa mikono na kuzingatia kutotangamana ili kudhibiti janga la virusi vya corona.

Picha aliyoiweka kwenye ujumbe wake imeripotiwa kubuniwa na kuwekwa mitandaoni na mtu mmoja raia wa Algeria asiyeamini Mungu mwenye makazi yake nchini Ufaransa.

Ujumbe huo wa Charqui uliwekwa wakati wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani huku Tunisia ikiwa inatekeleza masharti ya kutotoka nje.

Ujumbe huo ulisababisha ghadhabu mtandaoni huku watumiaji wa mtandao wakisema ni ujumbe wa kuudhi wakisema kuwa amejionesha wazi kuwa yeye si mtu anayemuamini Mungu wakitoa wito wa kuadhibiwa kwa Charqui.

Siku kadhaa baadae alihojiwa na polisi .

Tarehe 27 mwezi Mei taarifa zilisema kuwa Charqui anashtakiwa kutokana na chapisho hilo kwenye mtandao wa Facebook , huku Amnesty International ikitoa wito wa kufutwa kwa kesi dhidi yake.

''Mashtaka dhidi ya Emna ni ishara kuwa pamoja na kuwa Tunisia imepiga hatua katika masuala ya demokrasiia, mamlaka zimeendelea kutumia sheria za kukandamiza dhidi ya uhuru wa kujieleza,'' Mkurugenzi wa Amnesty International Kaskazini mwa Afrika, Amna Guellali alisema.

Bi Guellali ameitaka serikali ya Tunisia kubadili sheria hiyo ''ili iweze kuendana na haki za binadamu

Chanzo: BBC